Rutshuru : Wakaaji wa usultani wa Bwito ni wenyi furaha kutokana na FARDC kuuwa wajangili wawili

Eneo la Rutshuru.

Raia wa huko Kirima ndani ya usultani wa Bwito ni wenyi furaha chungu tele kwa kuwa askari jeshi FARDC waliweza kuwauwa jangili wawili waliokuwa wakinasa wapita njia kwenyi barabara Kibirizi Kikuku.

Duru za mahali hunena kwamba watenda maovu hawo walikuwa wakifyatuliya risasi kwa yeyote yule asiye heshimu amri yao .

Jambo lililopelekea kujitokeza kwa askari jeshi wa taifa na kuteketeza watenda maovu hawo, kwa kuwauwa.

Tufahamishe kwamba wiki iliyopita, mpiga picha moja alipata jeraha akigongwa risasi na watu hawo wenyi nia mbaya katika Kijiji cha Ngirima.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire