
Prezidenti wa Muungano wa wandishi habari jimboni Kivu ya kusini Darius KITOKA alikutana na wandishi habari juma tano tarehe 9 februari 2022 mjini Bukavu. Ni katika lengo la kujulisha mabadiliko yaliyo tarajiwa pamoja katika sekta ya habari na mawasiliano nchini DRC
Huyu anena pia kwamba mkutano wa pamoja sekta ya habari na mawasiliano ulisisitiza kwa jumla kuhusu kuboresha kazi ya upashaji habari. Shurti kwa kufanya kazi hiyo, kwa kutolewa kitambulisho cha kazi yaani kadi na mengineo.
Katika kikao iliombwa kwa Muungano wa wapasha habari UNPC kukaa pamoja ili kusaficha kinaganaga sekta hiyo, kutekeleza kanuni na vikartasi vya sheria vitaweza kuongoza kazi.
Prezidenti wa Muungano wa wandishi habari UNPC/ Kivu ya kusini aeleza pia kwamba kikao kilihusu siasa mhimu katika sekta ya upashaji habari na mawasiliano nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Darius KITOKA aongeza kuwa kikao hicho cha pamoja kati ya wandishi habari na serkali katika sekta hiyo kitafanyika mara tena ili kuweka nukta kwa azimio mhimu zilizochukuliwa hapa na pale. Ndipo sheria ya kudumu itatekelezwa.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.