Kivu ya kusini :Tomy Tambwe aomba wapiganaji mai mai kujisalimisha ili kujenga amani

Tomy Tambwe mratibu husika na kupokonya silaha makundi ya wapiganaji nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo amekutana na wakilishi wa makundi arubaini ya wapiganaji mai mai mjini uvira akitaka wajisalimishe.

Moses Simba akiwakilisha kundi moja la wapiganaji wenyi kuendesha kazi wilaya za Uvira, Fizi na Mwenga anena kwamba wametaka kuwe na amani ili yaonekana kwamba serkali haijakuwa tayari kutekeleza amani.

Kiongozi huyu wa wapiganaji aongeza kuwa walikwenda huko Murhesa Siku kadhaa katika mazungumzo ya kutaka amani itekelezwe ila hakuna kilicho fanyika upande wa serkali.

Naye mratibu husika na kuwapokonya silaha nchini Tomy Tambwe anena kuwa muda umepita tangu mazungumzo ya kwanza bila kufikia lengo. Akiomba wapiganaji kusema kipi kifanyike ili kutekeleza amani, na kufanya kazi za maendeleo maeneo hayo, akisisitiza kuhusu masikilizano.

Mkuu wa tume ya umoja wa kimataifa nchini DRC Kivu ya kusini ana matumaini kwamba kazi hizo zitafaulu tofauti na hapo awali.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire