Duru za karibu zake liwali wa Jimbo la Kivu ya kusini zaeleza kwamba Théo Ngwabidje Kasi, liwali wa jimbo la Kivu ya kusini, amechunguza hii juma mosi tarehe 4 juni 2022, kazi za ujenzi wa barabara zinazo fanyika jimboni. Ni katika kutayarisha ujio wake mfalme Philippe wa Ubeljiji tarehe 13 juni, ambaye anangojewa juma pili tarehe 12 juni 2022.
Kwenyi barabara nambari 5, yenyi kuelekea uwanja wa ndege wa Kavumu, alichunguza binafsi jisi kazi zaendelea hapa na pale mbele ya kuweka kabulimbu eneo hilo lenyi umbali wa kilomita sita. Kazi zikiendeshwa na shirika la ujenzi SOCOC, katika maoni yake Raisi wa DRC, kwa utetezi wake Théo Ngwabidje Kasi liwali wa jimbo.
Huyu atowa shukrani kwake Raisi wa DRC, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alijibu kwa ombi la raia, wakingojea pia ujenzi wa uwanja wa Kavumu.
Pamoja na hayo, liwali alitembelea pa Kalambo akicunguza upande huo wa barabara inayo pelekea pa ITA. Huku kazi za kukarabati barabara zitaanzishwa hapa karibuni, Kwa usapoti wa serkali ya jimbo, zikitekelezwa na shirika OVD, na kuungwa mkono na shirika SOCOC. Liwali alisisitiza kazi nzuri zifanyike na kwa haraka, kwa kuwa ni mwanzoni.
Théo Ngwabidje alihitimisha ziara yake mjini Bukavu kunako nafasi zingine za ujenzi wa barabara, mbele ya kwenda katani Panzi , ambako kazi zingine zafanyika. Ni tangu nafasi Maison blanche hadi kwenyi lupango ya ma padri Solidarité, barabara nambari tano na kuhitimisha kunako Cité de la joie.
Liwali wa jimbo akiomba viongozi wa mji na hata administreta wa wilaya ya Kabare, kuondowa kwenyi barabara gari zenyi kucakaa na vinginevyo barabara Kavumu hadi mjini Bukavu. Hatua inahusu pia wacuuzi kunako soko bandia, na hata wenyi kucuuza mcanga nafasi hiyo.
Liwali alisindikizwa na wanamemba wa shauri la usalama jimboni, pamoja na timu lililotangulia ajili ya matayarisho ya ujio wake mfalme Philippe wa Ubeljiji.
P.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.