DRC : Mgomo wa waganga wakuu waendelea ijapo mazungumzo na ngazi za Raisi wa taifa

Waganga hawa walipokelewa hii juma tano tarehe 5 oktoba 2022 naye kiongozi wa ofisi ya Raisi wa taifa Guylain Nyembo. Mazungumzo iliyofanyika kwa siri, kunako Cité de l’Union Africaine mjini Kinshasa.

Baada ya mazungumzo, prezidenti wa shirika la kutetea haki za waganga SYNAMED John Senga aeleza kwamba mazungumzo hayo na kiongozi wa ofisi ya Raisi, ilikuwa namna ya kutafuta kukutana ana kwa ana na Raisi wa taifa binafsi Félix Antoine Tshisekedi.

« Siyo kusema tunakomesha mgomo. Mgomo inaendelea hadi Raisi wa nchi atakapoleta suluhu kwa malalamiko yetu » , anena kiongozi wa shirika la kutetea haki za waganga SYNAMED John baada ya kukutana na kiongozi wa ofisi ya Raisi.

Tukumbushe kwamba ni tangu mwezi julai 2022 ndipo waganga wakuu waliweza kuanza mgomo, wakiomba serkali kuwahudumia vilivyo kikazi na kijamii. Na wakati wa maandamano siku zilizopita, hawa walisambazwa na walinzi wa usalama. Hiyo ikasababisha majeraha kutokana na bomu za kutowa machozi.

Juvénal Murhula.


.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire