Maandamano iliyoandaliwa na vijana mjini Lubumbashi jimboni Katanga, imepigwa marufuku na waziri wa mambo ya ndani jimboni humo. Ilikuwa hii ijumaa tarehe 14 oktoba 2022.
Askari polisi waliwekwa kwenyi mashanganjia na pembe zote za mji saa za alfadjiri, ili kupinga kila hali ya maandamano kwa vijana wa jimbo hilo.
Duru toka Lubumbashi zaangazia kwamba ni maandamano mbili iliyokuwa ikipangwa , kati ya chama UDPS na Ensemble pour la République. Vijana wa UDPS wakilazimisha Ensemble pour la République iondoshwe ndani ya muungano Union sacrée. Ni kutokana na matamshi yake mnenaji wa Moïse Katumbi, Bwana Olivier Kamitatu ambaye alinena kwamba hawata vumilia wizi yoyote toka uongozi ulio madarakani. Upande mwengine, vijana wa Ensemble pour la République wasema kuendelea kuunga mkono Moïse Katumbi.
Ndipo waziri wa mambo ya ndani alikataza maandamano hizo akiogopa vinyume vitaweza jitokeza.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.