Kinshasa : Misa imesomwa kwa kuwakumbuka ma mia ya wakongomani waliouliwa na waasi wa M23 pamoja na Rwanda.

Misa ilisomwa hii juma tano tarehe 7 disemba 2022 kwenyi parokia sacré cœur mjini Kinshasa, ili ya kuwakumbuka wakongomani mia 272 waliouliwa kinyama na waasi wa M23 wakisaidiwa na Rwanda. Jambo lilifanyika pa Kishishe wilayani Rutshuru, juma lililopita.

Msemaji wa serkali ya DRC, Patrick Muyaya anena kwamba misa iliyosomwa ni ajili ya kupongeza jamaa za wahanga waliouliwa. Pia kukumbusha sheria ambayo imeanza kufanya kazi, kuendelea ili walio sababisha machafuko hayo waazibiwe kulingana na makosa yao. Akiongeza kwamba ni namna ya kualika wakongomani kwa Umoja.

Walishiriki kwenyi ibada hiyo, viongozi kadhaa wa Jimbo la Kivu ya kaskazini, yaani yaani wanabunge, mawaziri, na viongozi wengine wengi toka jimbo hilo.

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire