Goma: Mji wa Goma uko hatarini kiuchumi kwa kuvamiwa kwa Bunagana na penginepo na waasi wa M23

Watetezi wa haki za binaadam wilayani Rutshuru waangazia kuhusu shida ambayo inakumba kiuchumi mji wa Goma, kutokana na kuvamiwa kwa Bunagana na penginepo na waasi wa M23. Wakiomba viongozi kufanya yote iwezekanayo ili kukomesha hali hiyo.

Aimé Mukanda moja wa waheshimiwa wilayani Rutshuru ataja mfano ya wanafunzi wilayani humo, ambao ni wahanga kutokana na vita vyenyi kuwatenga na mji wa Goma.

Huyu aangazia kwamba hali yatasababisha mauaji ya kimbari humu jimboni, mfano wa machafuko iliyofanyika nchini Rwanda mwaka 1990-1994. Kwa kuwa wanaofanya vita nchini wilayani Rutshuru , ni wale waliofanya mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Mwana memba huyu wa shirika la raia akizungumza na wenzetu wa le quotidien.com, aonyesha kwamba waasi wa M23 wapenda kuvamia zaidi maeneo zenyi madini yaani Rubaya, Masisi na Somikivu. Akiomba viongozi kucunguza vema vyombo vya upashaji habari nchini, hasa habari za vita. Pia kuvunja uongozi wa kijeshi na kutaja rasmi jimbo la Kivu ya kaskazini lenyi kukumbwa na maafa.

Chumba cha waandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire