Kivu ya kaskazini : Zaidi akina mama mia wahami wa vita wanaokaa pa Nyiragongo waomba Raisi wa taifa usalama ili warudi makwao

Zaidi ya akina mama mia wahami wenyi kukaa pa Nyiragpngo waliandamana mjini Goma hii ijumaa tarehe 17 februari 2023, wakilaumu usalama mdogo makwao, kutoka waasi wa M23. Pamoja na hayo, kutojiunga kwa vikosi vya EAC na jeshi la taifa ili kufukuza waasi wa M23.

Kwenyi vitambaa walivyo vipeleka: « Tunakataa usalama mdogo. Tshisekedi fungua milango turudi kwetu » wakitowa maxhozi.

Kibarua  kilicho somwa mbele ya wandishi habari  kinaonyesha kwamba watu 482 waliuliwa na waasi wa M23. Miongoni mwao akina mama 185 na watoto 88. Wengi miongoni mwa wahanga waliuliwa pa Rwanguba, Ruvumu, Rugari, Kinyandonyi, Bambo, Kishishe, Kisharo, Ruseke, Kahumiro, wilayani Rutshuru, na wengine Nyiragpngo na Masisi.

 » Machafuko ya hapa karibuni  ni pa Birambizo hii tarehe 14 februari 2023. Raia 5 waliuliwa kunako hospitali, na parokia moja kuporwa. Miongoni mwa wahanga akina mama wawili wazee, moja akiwa na umri wa miaka 60 na mwengine miaka 70. Wakibakwa mbele ya kuuliwa na waasi wa M23. Mganga moja naye kuuliwa, vituo 11 vya afya kuporwa na waasi, ambayo ni mauaji ya kimbari » wakinena akina mama hawo.

Hawa waomba serkali kufukuza waasi wa M23 kwa haraka iwezekanayo, ili amani irudi. Waweze kurudi makwao na kujiorodhesha kuhusu harakati za uchaguzi. Kwa mahakama ya kimataifa, akina mama hawo waomba kifungo kwa wahusika katika machafuko ya waasi wa M23, na walipe kila walicho kiharibu.

Tufahamishe kwamba  maandamano ilianza pa Nyiragpngo, kupitia INSTIGO, Entrée Présidentielle, hadi kwenyi ikulu ya liwali, ambako mwakilishi wake aliweza kupokea kibarua. Akiahidi kukipokeza kwa mhusika.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire