Kivu ya kaskazini : Jules Lubungo Matayo aomba iongezwe muda ya orotha ya wachaguzi

Tume huru ya uchaguzi CENI iongeze mwezi moja hadi tarehe 15 mei 2023, ili kuorodhesha raia wote wilayani Nyiragongo hususan katika kijiji Kiziba2. Kupata kadi ya mchaguzi kwa kila mkongomani ni haki, siyo msaada.

Jules Lubungo Matayo moja wa viongozi wa kijiji Kiziba2 na mwanzilishi wa Fondation Jules Lubungo Matayo alinena hayo akihojiwa na mwana ripota wa la ronde info mjini Goma. Ni baada ya mzunguko kwenyi senta kadhaa za Kiziba2, ili kuchunguza jisi kazi zafanyika kutokana na malalamiko mengi ya raia.

<<Kutokana na jisi orotha ya wachaguzi inafanyika ndani ya eneo langu Kiziba2, na kwa kuwa imetangazwa kuhitimisha Operesheni juma nne, nazani raia wataweza tutupia mawe. Asilimia 50 hawaja pata kadi ndani ya eneo Kiziba2 hadi sasa, Niliwahi kutembelea senta zote eneo la Mudja. Kwa uhakika, shida ni chungu tele. Watu hushutumu watumishi wa CENI kuomba rushwa. Hatuwezi kataa ama kukubali, kwa kuwa sijaona binafsi,>> aeleza Jules Lubungo.

Akigusia pia hesabu ndogo ya kampyuta ndani ya senta, hiyo inapelekea kazi kwenda kwa mwendo wa kobe. Kompyuta mbili ama tatu kwa senta moja, ijapo hesabu ya raia Kiziba2 ni zaidi ya elfu 40 na elfu 50.

<<Tunaweza kuwa na idadi ya watu elfu 40 ama elfu 50. Wakingojea orotha kupitia kompyuta mbili ama tatu muda wa mwezi moja. Nani aorodheshwe na nani aachwe. Kwa jumla ni watu 200 na 250 kwa siku. Mara kwa mara kompyuta zinaharibika. Kosa ni la nani . Kijiji Kiziba2 inahitaji kompyuta sita ili kurahisisha kazi. Inaomba kuongeza mwezi moja ili kila mtu aorodheshwe. Ni kusema hadi tarehe 15 mei 2023, watu wote watakuwa wamepata kadi zao>>, afasiria Jules Lubungo Matayo moja wa viongozi wa kijiji Kiziba2 na mwenyeji wa shirika lenyi kuitwa kwa jina lake.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire