Kivu ya kaskazini : Utawala wake Félix Antoine Tshisekedi waonekana kushindwa uongozi wa nchi ( Promesse Matofali)

Akitokea ziarani mjini Kinshasa, Ituri, Tshopo na Kivu ya kaskazini, mwanabunge wa jimbo la Kivu ya kaskazini Promesse Matofali anena kwamba kazi za chama cha kisiasa Ensemble pour la République zaendeshwa vizuri. Na kwamba Prezidenti wa chama hicho ,Moïse Katumbi ashutumiwa bila hatia, na utawala ulio madarakani ambao umeonekana kushindwa kazi.

Amenena hayo hii juma nne tarehe 30 mei mbele ya wandishi habari, kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma. Akihojiwa kuhusu shutuma kila leo dhidi yake Moïse Katumbi, mwanabunge Promesse Matofali anena kwamba hiyo ni alama ya kushindwa ya viongozi walio madarakani, wakitafuta sababu zisizofaa.

<<Unajua mtu akishindwa hutafuta sababu. Ukumbuke kwamba Adam na Eva walikula tunda ndani ya bustani ya Edeni . Mungu alipofika Adam akashutumu mkewe Eva, kwamba ni yeye aliweza mdanganya wale tunda . Eva naye akashutumu nyoka. Mtu anaposhindwa hutafuta sababu, kwa kufasiria kushindwa kwake. Munajuwa kwamba utawala wake Félix Antoine Tshisekedi umeshindwa kazi kinaganaga katika sekta zote; kiusalama, kiuchumi. Hakuna maoni ama mpangilio wowote ule kuhusu uongozi wa nchi,>> afasiria mwanabunge huyo.

Promesse Matofali aongeza kwamba raia wafahamu yote kuhusu uongozi mbovu ya serkali iliyo madarakani ikipapasa.

<<Sisi tunajiandaa vilivyo. Tunaandamana ili kulaumu uongozi mubaya ulioko nchini. Katika sekta za usalama na harakati za uchaguzi. Natoka mjini Kinshasa ambako nilishiriki kwenyi maandamano, tukikaa chini na kadhalika. Kunaandaliwa pia hotuba tarehe 17 juni, muda ambao upinzani utajieleza. Hatutachoka kufwatilia serkali iliyo madarakani na ambayo tayari imeshindwa kazi >>, asisitiza mwanabunge.

Promesse Matofali alijibu kwa maswala mengine, yaani kuwepo kwa vikosi vya ugenini nchini, yaani MONUSCO, EAC, na baadae SADEC ambavyo havikufaulu kutekeleza usalama. Jambo linalo mhusu Raisi wa taifa peke ambaye aliweza kualika vikosi hivyo . Uongozi wa kijeshi kwenyi eneo za Kivu ya kaskazini na Ituri, ambayo pia havikufaulu. Promesse Matofali aomba raia kuunga mkono askari jeshi wa taifa FARDC, askari polisi na hata wafanya kazi wa shirika la ujasusi, ajili ya kutekeleza usalama nchini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire