Goma: Baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa bunge la jimbo na la taifa raia wajiswali mengi

Matokeo ya uchaguzi wa bunge la jimbo na la taifa tayari imekwisha kutangazwa. Miongoni mwa raia kauli ni tofauti baada ya kutangazwa kwa matokeo. Wamoja wakionekana kutoelewa matokeo ambayo hawakungojea kama ilivyo kwa sasa. Wengine husema kwamba matokeo hayo ni halali kabisa, hata kama iliwarudisha mara tena wanabunge waliomaliza mhula. Na kwamba hawa wanastahili.

Wadadisi wa mambo kadhaa wajiswali je mabunge hawa wa jimbo na wa taifa watafanya kazi vilivyo ama ni bahati kwao kupokea pesa za serkali miaka tano ijayo peke bila kuchapa kazi . Wait and sée ngojeni tukaone wasema wangereza.

Wengine hutumainia mabunge hawa, wakiwa na matumaini kwa walio chaguliwa mara tena, kuwa wamepewa bahati mara tena ili wazidishe bidii ndani ya kazi, wakifanya zaidi kuhusu waliofanya wakati wa mhula umekwisha.

Wengi miongoni waliofanya chaguo hilo hawana uhakika kwamba wachaguliwa hawa watabadili mwenendo wa kazi, wakinena kwamba ni namna ya kuwapima mara tena kuhusu mhula huu. Na kwamba wabadilishwe siku za usoni wasipofaulu.

Ni kusema kwamba raia waliofanya chaguo hilo na wale hawakufanya wote wasema kungojea matumikio kwa watu hawa mara tena. Miongoni mwa raia wenyewe, wamoja wazani kuweza kula rushwa za makandideti ijapo wengine wamefanya chaguo lililo bora, yaani hawakukula rushwa.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire