Mwanabunge wa taifa mzaliwa wa jimbo la Kivu ya kaskazini Hubert Furuguta ameomba kwa sauti kubwa wenzake wafanya siasa toka mashariki mwa DRC, kuhusika binafisi na maswala yenyi kuwahusu. Akitupilia mbali kuwakilishwa na watu wa Kinshasa peke, ambao hawana uhakika kuhusu hali mashariki mwa DRC.
Huyu anena hayo ndani ya kikao kwenyi bunge mjini Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo
<< Hatupashwi kuanza mhula tukisinzia kama ilivyo mbeleni. Tuonyeshe ulimwengu nzima kwamba haraka yahitajika kutokana na hali ambayo yakumba DRC miaka mingi. Nchi kadhaa zajihusisha na shida za DRC ambayo inazorota. Kila mara twaomba misaada kwa wazungu ambao waunga mkono nchi jirani zenyi kutushambulia. Wafanya siasa, viongozi wa makabila, wasomi na Kivu yote kwa jumla amkeni. Tusiendelee kuwakilishwa na watu wa Kinshasa ndani ya vikao ugenini, ijapo hawafahamu shida zinazotukumba,>> asisitiza mwanabunge Hubert Furuguta.
Huyu anena kuwa wafanya siasa wenzao wa Kinshasa hawajue tofauti kati ya mshambulizi na mhanga. Akitaja mfano wa mji wa Goma, ambao washambuliwa kila leo na majambazi wasiojulikana mchana na hata usiku.
<<Ijapo shida, serkali jimboni na hata ile ya taifa, hakuna suluhu la kudumu. Wakijihusisha na swala kwa uzembe. Ndio maana wafanya siasa mashariki wakuwe makini kuhusu hali mbovu inayowakumba>>, aendelea kusisitiza mwanabunge Hubert Furuguta.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.