Nyiragongo : Vijana wa Kijiji Kiziba 2 wajihusisha na usalama pamoja na maendeleo makwao wakiomba serkali kuwaunga mkono

Prezidenti wa vijana wa Kiziba ya pili Adelard Amani Mulindwa.

Prezidenti wa vijana pa Kiziba 2 Akilimali Mulindwa Adelard , ahakikisha uhusiano kati ya vijana na mashirika za usalama makwao ijapo usalama kuzorota kiasi eneo hilo.

Huyu aongeza kuwa ripoti zatolewa kila leo kwa askari polisi, askari jeshi na hata kwenyi shirika la upelelezi, ila visa vya usalama mdogo ni chungu tele eneo hilo.

Kiongozi wa vijana kijijini Kiziba 2 asema kuwa watu hunyanyaswa, kupigwa, wizi wa kila aina na vitendo vingine vya kinyama watendewa. Huyu aongeza kwamba hata kama idadi ya walinzi wa usalama ni ndogo, ingibidi juhudi na hata alama ya kutaka kutekeleza amani vinaonekane upande wa husika.

Adelard ataja mfano wa kisa cha wizi kilicho fanyika nyumbani kwa kinamama moja ambaye aliibwa hata mavazi ya mtoto mcanga kabla hajafika nyumbani toka hospitali alipokwenda zaa na mengineo.

Kuhusu maendeleo ya vijana wa mahali, prezidenti huyu aligusia mashindano ya mpira wa kandanda walioandaa eneo mwezi julai, namna ya kupiganisha hali ya kuzurura kwa vijana. Pamoja na mazoezi mengine yaani ngumi, vipasi na kadhalika.

Na kuhusu kazi za usafi, Adelard afahamisha kwamba vijana wa Kiziba 2 hujitahidi kwa kazi za usafi ila ukosefu wa vyombo vya kazi. Huyu aendelea kuomba serkali awaunge mkono kwani hawatafaulu wenyewe.

Kwa vijana wenzake aliwaom ba kuepuka nafasi za vileo, yaani pombe za kulevya na bangi. Pia waepuke vitendo vya ugaidi, wizi na kadhalika. Akialika vyombo vya usalama kwa uhusiano bora na raia ili kuteketeza amani ya kudumu makwao.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire