Goma: Raia watolewe silaha ili kujikinga kutokana na kuzorota kwa usalama kiasi nchini DRC ( Promesse Matofali)

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Promesse Matofali.

Raia wapewe silaha nchini DRC kulingana na hali ya usalama yenyi kuzorota kila leo humo. Ni pendekezo la mwanabunge Promesse Matofali kwake Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO wakati wa kikao na wanabunge wa jimbo ishirini na sita mjini Kinshasa.

Mwanabunge Promesse Matofali anena hayo mbele ya wandishi habari hii juma nne tarehe 22 machi kwenyi uwanja wa ndege pa Goma akitokea mjini Kinshasa.

Huyu aangazia kuwa tangu tarehe 10 hadi 17 machi ni raia 79 ndio wameuliwa, wakiongezeka kwenyi idadi ya 2068 ambao wamekwisha uwawa tangu mwezi mei iliyopita, ndio maana inabidi kila raia atolewe silaha kwa kujichunga.

 » Tukiangalia ndani ya nyumba zetu tunazo mipanga na hata visu. Tuna vitu vingi ambavyo ni silaha za asili. Na kwa nini raia hawavitumikishe kwa kuuwana. Ni kusema watu wasiwe na hofu juu ya kumupa mutu silaha ili aweze jikinga kwa maadui wenyi kuwauwa watu pa Béni na penginepo, anena mchaguliwa wa Béni.

Akiendelea kuomba raia wasiwe na hofu kwani kulingana na mpango huo serkali itaweza kuchunguza na kujuwa hesabu ya silaha alizozipewa kila mtu.

Sisi tunasema jeshi la DRC liko linafanya kazi likisaidiwa na lile la Uganda. Pamoja na hizo mbinu zenyi kuchukuliwa na serkali, itowe silaha pia kwa raia mfano wa nchi ya Ukraine ambayo inaendelea kupinga jeshi la Urusi, atamka Promesse Matofali. Akihitimisha kwamba jambazi anapokaribia atapigwa kwa silaha na yote yatakoma.

Juvénal Murhula..

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire