Kivu ya kusini : Raia waonekana kuchoka wakingojea aachiliwe huru Prezidenti wa chama cha kisiasa UNC Vital KAMERHE

Katibu makamu wa chama UNC jimboni Kivu ya kaskazini anena kuwa raia wamengojea siku si nyingi kuachiliwa kwake prezidenti wa chama chao UNC Vital KAMERHE ila hakuna kilicho fanyika hadi sasa . Kwa hiyo chama hicho kinaandaa kazi kadhaa namna ya kutoa malalamiko kwa kuomba afunguliwe Vital KAMERHE.

« Haiwezekane tarehe nane aprili na mwezi yote kupita bila kufanya chochote kile . Ni kusema kuanzia hii alhamisi tarehe nane aprili chama cha kisiasa UNC kinaandaa kazi kadhaa kazi katika hali ya amani mfano wa misa, na ibada mbali mbali ili kumuweka prezidenti wao Vital KAMERHE mikononi mwa Mungu muweza yote « anena kiongozi huyu Daniel Lwaboshi.

Duru zetu kutoka mjini Bukavu zaeleza kuwa Daniel Lwaboshi aligusia pia kazi za kongamano, mazungumzo kati ya raia , matendo kuhusu upendo , yote katika lengo la kutafuta aachiliwe huru Prezidenti wa UNC Vital KAMERHE.

Daniel Lwaboshi aongeza kuwa raia wameonekana kuwa wameanza kuchoka kuona siku zaendelea bila kupata suluhu kwa shida yao.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire