Goma: Jumba za byashara ndani ya soko ya viato CADECO MAENDELEO zimewaka moto

Zaidi ya wafanya biashara mia tano , miongoni mwao wengi ni akina mama wachuuzi wa viato kwenyi soko CADECO MAENDELEO wamepoteza byashara yao. Ni kutokana na moto iliyojitokeza majira ya saa kumi na mbili na nusu, hii juma pili tarehe 10 disemba 2022.

Mama Atosha Micheline prezidenti makamu wa wachuuzi ndani ya soko hiyo anena kwamba ni jambo lenyi kushangaza, ingawa kuna mizozo kati muungano wao,  na akina mama mwenzao aliyependa aondoka ndani ya muungano.

« Jambo la kushangaza ni kwamba kulikuwa mizozo kati ya sisi wachuuzi. Kuna mama moja kati yetu ambaye alijiondowa kati yetu na kuunda kikundi ya kwake. Hatujuwe kama ni yeye angelitenda jambo hili. Moto iliwaka majira ya saa kumi na mbili na nusu. Watu wasiojulikana walijitokeza na kumpiga zamu kama nyoka, hadi kupoteza fahamu . Baada ya hapo, moto ukawaka kiasi na kuchoma jumba ambamo tunaweka biashara. Hatujuwe kama ajali hiyo inatokana na kesi kwenyi mahakama ya kijeshi kati yetu na akina mama huyo aliyejitenga. Pia siku mbili baada ya mama huyo kuondowa byashara  yake ndani ya jumba, ndipo ziliwaka moto , »  aendelea kujiswali Bi Atosha Micheline.

Bi Atosha Micheline aomba viongozi wa nchi kuwahudumia kwa kuwa jamaa zao zapatakina hatarini kwa sasa, zikikosha chakula na hata shule. Vitu vilivyo waka moto ni viato, mafuta ya kupakaa, vifa vya ujenzi, begi na kadhalika.

Wachuuzi wengine wengi tulio wakuta nafasi ya ajali, waliendelea kulilia serkali aweze kuwatoleya msaada kutokana na shida  inayowakumba. Wakiwa wenyi kushangaa jisi ajali iliweza jitokeza.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire