Goma: Mwanabunge Adele Bazizane aomba raia wa Nyiragongo kutoa malalamiko ili kuyafikisha kwenyi ngazi za juu na kutafuta suluhu

Mwanabunge Adele Bazizane akitokea mjini Kinshasa

Akitokea mjini Kinshasa hii ijumaa tarehe 18 juni 2021 Mwanabunge Adele Bazizane aeleza kwamba alikwenda kushiriki kwenyi semina iliyo husu kupiganisha kutopewa uraia.

Akialikwa pamoja na wenzake wa majimbo za Kivu ya kusini, Kasaï ya kati na Tanganyika.

« Mwafahamu hali ya kutokuwa na uraia ni kutojulikana kama mwanainchi ndani ya nchi. Jimboni Kivu ya kaskazini, kuna maendeleo kuhusu swala hilo , kwani nilipokuwa waziri wa jinsia nimefanya uhamasishaji dhidi ya akina mama wafanya biashara Goma Gisenyi. Wakati huo tuliorodhesha watoto wengi na tunashukuru Julien Paluku aliyekuwa liwali kwa kuturahisisha kazi wakati ule » asema Adele Bazizane

Pamoja na hayo Mwanabunge huyu anena akutanana na viongozi kadhaa mjini Kinshasa katika lengo la kutetea Jimbo la kivu ya kaskazini na hata wilaya yake ya Nyiragongo ambayo yeye ni mcanguliwa. Akigusia hasa usalama mdogo na mripuko wa moto wa volkeno Nyiragongo.

« Tunaamini kwamba amani itarejea jimboni Kivu ya kaskazini, na hii ni kilio cha kila yeyote na hata wabunge jimboni humo. Nasisitiza kuhusu Nyiragongo eneo iliyoni chaguwa . Mwafahamu kwamba mripuko wa volkeno tarehe 22 mei iliharibu upande moja wa Nyiragongo. Nilikwenda ona waziri wa elimu na kumuelezea kwamba kuna watoto wengi waliopoteza buku, vibao na kwamba wazazi hawana makao kwa sasa » anena Adele Bazizane mbele ya wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma.

Akigusia swala kuhusu mtihani wa serkali kwa kuwa wazazi hawana chochote cha kulipa.

« Waziri amesema atatia mkazo kuhusu swala hilo na kulazimisha viongozi jimboni Kivu ya kaskazini waache watoto wilayani humo kufanya mtihani bila shaka » aendelea kunena mcanguliwa wa Nyiragongo

Mwishowe alitowa pôle kwa wote waliopoteza wakati wa ajali ya moto , hasa kwa wote waliopoteza ndugu zao. Pia kushukuru Raisi wa DRC, serkali na washirika wengine kujihusisha kinaganaga katika swala kuhusu usalama, na huduma kwa wahami wa moto wa volkeno Nyiragongo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire