Goma: Shirika lisilo la kiserkali OILICE latoa shurti kwa serkali kwa kuondoa sheria yenyi kukinga hukumu ya kifo

Katika mkutano na wandishi habari kwenyi jumba la wandishi habari UNPC mjini goma, shirika lenyi kutetea haki ya binaadam OILICE lanena kutoegemea upande wowote ule kuhusu hatua iliochukuliwa na serkali ya Drc. Hatua inayoonyesha kuondolewa kwa sheria yenyi kukinga hukumu ya kifo nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Likitowa shurti kadhaa kwa kusindikiza hatua hiyo ya serkali.

<< Shirika lisilo la kiserkali OILICE latumika kwa kupiganisha rushwa na na kuimwa sheria.  Ndipo lilipenda kuleta maoni yake kuhusu kuondowa sheria inayokinga hukumu ya kifo kwa serkali ya DRC. Shirika hili halitegemee upande wowote, halilaumu na hata kumsindikiza mtu yeyote. Ila latoa pendekezo ili kusindikiza hatua iliyochukuliwa na serkali ya DRC, anena mratibu Gladis Kingombe wa shirika OILICE.

Huyu anena kwamba inabidi hukumu ya kifo iwe mfano kwa watu wote, hata kwa wafanya siasa. << Kwani afisa moja wa kijeshi hawezi kuwa na uhusiano na nchi yenyi kushambulia ingine, ingawa hakuna uhusiano na viongozi wa kisiasa. Pamoja na hayo, yeyote atachukuwa silaha kwa kupiganisha nchi yake, aondolewe uraia kama mkongomani. Hiyo itampelekea kutotenda maovu yoyote kwa jina la taifa. Pia shirika hili laomba serkali kutotundika vijana wanaponaswa, kwa kuwa ujambazi mjini unasababishwa hasa na vijana wasio na kazi, aeleza kiongozi huyo.

Mwanasheria Gladis Kingombe kupitia shirika OILICE aomba serkali kuunda kazi ajili ya vijana, kwa kuwa ni jukumu lake. Na kwamba vijana ni asilimia themanini miongoni mwa raia kwa jumla na wengi hawana kazi.  Serkali iweze kushusha pia kodi na ushuru, ili kuruhusu vijana kuunda wenyewe kazi.  Wakitolewa pia mafunzo.

Shirika lenyi kutetea haki ya binaadam OILICE laomba serkali kutangaza kwenyi runinga ya taifa kesi ya mtu anayeshakiwa kuhojiana na magaidi wa M23 ama waasi wengine. Pahali pa kutangaza haraka kwenyi vyombo vya habari akiwa kifungoni.

Katika kikao hicho na wandishi habari, shirika hili lilitangaza pia ripoti ya utafwiti liliondesha wakati wa harakati za uchaguzi wa disemba 2023.  Huku likionyesha makosa ilionekana hapa na pale wakati huo. Na kwamba kuziepuka munamo siku za usoni. Ingawa kuna mambo kadhaa iliofaulu wakati ule. Viongozi wa shirika OILICE walijibu moja kwa moja kwa maswala ya wandishi kulingana na nukta zilozungumziwa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire