DRC : Raia wajiswali kuhusu matokeo ya serkali nyipya itakoyo tangazwa ambayo yafanana kuota mizizi

Juvénal Murhula mwandishi mwanzilishi wa la ronde info,com

Raia walio wengi nchini DRC waanza moja kwa moja kukata kitumaini kuhusu serkali nyipya toka utawala wake raisi Félix Antoine TSHISEKEDi ambayo ni kama wahenga husema : « Ngombe ya maskini haizae ».

Ni tangu miaka chungu tele, zaidi ya asilimia themanini ao tisini ya wakongamani wakumbwa na matatizo ki usalama, ki uchumi, kijamii, kisiasa na kadhalika.

Wadadisi wa mambo walikuwa wamezani kwamba utawala huu wa sasa ni suluhu kwa shida wazipitia wakongamani kutokana na ahadi zilizotolewa kila leo , yaani shule kwa bure. usalama wa kudumu, mishahara inayofaa kwa jumla yenyi kujibu kwa shida zinazokumba wakongamani.

Wadadisi wa mambo hawa waendelea kujiswali , kwa nini ngombe ya maskini haizae?

Serkali inayo ngojelewa imekwama ama watakayoiongoza wapo wakipigania mkate kama ilivyo desturi ya serkali za hapo mbeleni? Ni nani miongoni mwa viongozi wa sasa anavaa ngozi ya raia wanaoteketea kulingana na maisha mabovu waishimo?

Hawa waendelea kujiswali ni nani Musa wa DRC, atatoka wapi ili wakongamani wapate haki yao kulingana na sheria ya nchi?

Wataalam wengine hunena kwamba uongozi wa DRC washurtishwa na utawala wa wazungu ijapo mzungu anapotowa misaada si yeye atawafunza kumpenda ndugu zao wanainchi na kujuwa kama wana haki kama wao

Wataalam hawa wazani kwamba DRC haitendelea kamwe viongozi wasipo acha kujipendelea wenyewe wakiiga hata mfano wake hayati John POMBE MAGUFULI aliye kuwa raisi wa Tanzania . Kama sivyo raia waweze kujitegemea kama anena kila leo mfanya siasa Jimboni Kivu ya kaskazini Profesa Daktari Dady SALEH.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire