Bukavu : Mwanabunge moja kupigwa vikali na mpasha habari kujeruhiwa wakati wa maandamano kwenyi uwanja wa Funu

Watu sita wamejeruhiwa miongoni mwao mpasha habari ila mwanabunge kupigwa mjini Bukavu hii juma tano tarehe 18 aprili 2021 kunako uwanja wa Funu.

Kutokana na duru zetu hayo ni matokeo ya mkutano wa hazarani ulioandaliwa wanabunge waliosaini barua ya kumuondowa madarakani liwali wa Jimbo la Kivu ya kusini Théo Ngwabidje Kasi.

Duru za mahali zanena kuwa askari polisi wazaniwa kufyatulia raia risasi ili kusambaza waandamanaji .

Hawa waliendelea kupinga hadi kupelekea majeraha.

Duru zaendelea kuhakikisha kwamba miongoni mwa walio jeruhiwa mpasha habari wa redio n’a televisheni Canal futur pamoja na mwanabunge jimboni.

Tufahamishe kwamba waliojeruhiwa walipelekwa kwenyi kituo cha afya cha karibu ili kutolewa matibabu.

Chumba cha wahariri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire