Goma: Wanabunge nane wa Jimbo la Kivu ya kaskazini wakuja kuchunga hali ya usalama jimboni mwao

Wanabunge nane wa Jimbo la kivu ya kaskazini wako ziarani mjini Goma ili kujionea binafsi hali ya usalama jimboni humo.

Muda murefu walikutana Jana juma pili na liwali wa Jimbo hilo Carly Nzanzu Kasivita kuhusu hali ya usalama mdogo inayo kumba Jimbo siku hizi hasa hali ya heka heka iliyo pelekea watu kumi kuuliwa na kuchomwa moto kwa nyumba Nyiragongo na kando ya mji wa Goma.

Kutokana na mwanabunge Didier Kamundu ambaye anaongoza ujumbe ,waliweza kuja ili kukutana raia ili kujuwa jukumu la kila mutu katika machafuko iliyo endeshwa kwenyi eneo hilo la Jimbo la Kivu ya kaskazini.

Baada ya kukutana na liwali wa Jimbo, wabunge hawo waliahidi kuunga mkono liwali wa jimbo ambaye apigana kuhusu usalama wa Jimbo la Kivu ya kaskazini.

Tufahamishe kwamba wanabunge ni Didier Kamundu, Hubert Furuguta, Patrick Munyomo, Jeannette Mapera, Jean Baptiste Kasekwa, Josué Mufula, Elvis Mutiri na kadhalika.

Juvénal Murhula

1 Comment

Poster un Commentaire