Goma : Carly Nzanzu Kasivita aondosha kazini mashauri wake ahusikae na mambo ya sheria katika mizozo ya uwanja SOTRAKI

Paluku Matofali Guy Richard mashauri wa mambo ya sheria wake liwali ameachishwa kazi naye liwali mwenyewe Carly Nzanzu Kasivita . Akishutumiwa ndani ya ujanja uliozusha migogoro kati ya meja Kizito Nshokano na vijana wa kata Kyeshero wakishuka barabarani.

Katika barua yake liwali huyu ashutumiwa mambo mengi: Kwanza kusaini makubakiano ya kwanza kuhusu uwanja SOTRAKI kwa jina la liwali bila kumjulisha.

Jambo la pili kusindikiza pande husika ndani ya mizozo kwa jina la liwali akisaini makubaliano ya kwanza ilio pelekea kuanzishwa kwa kazi.

Barua hiyo imesainiwa naye kiongozi wa ofisi ya liwali wa Jimbo kwa jina la Jean Paul Kahindo Maregani yaeleza kuwa hayo yote yalifanyika katika hali ya rushwa na uongo.

Ndio maana kuanzishwa kwa kazi eneo hilo ilipelekea hali ya heka heka eneo , vijana wakipinga ujenzi wowote ule nafasi pale.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire