Goma : Mwanabunge Safari Nganizi na wachaguliwa wake wangojea usalama kwa serkali nyipya

Akiwa ziarani jimboni Kivu ya kaskazini mwanabunge Safari anena kuja jimboni Kivu ya kaskazini ili kuzungumza na wachaguliwa wake kuhusu yale wangojea kwa serkali nyipya yake Sama Lukonde kwa kuwa hakupata muda ya kufika wakati wa likizo . Ni muda kwake kujitokeza .

Alinena hayo mbele ya wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma akizungukwa na wafwasi wa chama chake .

« Tuko siku hizi katika kikao bungeni ila nafika jimboni kwa kuwa sikufika wakati wa likizo . Mwafahamu kwamba tayari serkali nyipya imetajwa. Nakuja ili kuzungumza na wachaguliwa wangu kuhusu kazi ambayo serkali inabidi kufanya kwa manufaa ya raia . Mwajuwa kwamba Jimbo la kivu ya kaskazini lakumbwa na usalama mdogo: Masisi, Beni, Rutshuru na penginepo . Hata kama hali ya fanana kuwa shwari mjini ila huko nje ni hali ya heka heka » anena mwanabunge.

Mwanabunge mcanguliwa wa Masisi amesema kuunga mkono serkali ya pamoja yaani union sacrée kwa kimombo maana ilikuwa miaka mbili tangu uongozi bila matukeo.

Mwanabunge huyu ambaye pia prezidenti wa chama PARECO aomba wachaguliwa wake kuunga mkono serkali ilioko na hata maoni ya Raisi wa DRC, ili kurejesha usalama mashariki mwa DRC hususan jimboni Kivu ya kaskazini ambayo yakumbwa n’a vita miaka chungu télé

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire