Kivu ya kusini : Swedy BASILA atoa muda wa mwezi moja kwa watembeza pikipiki na madreva ili kununua vikartasi mhimu vya kazi

Waziri wa uchukuzi jimboni Kivu ya kusini ametoa mwezi moja kwa watembeza pikipiki na madreva mjini Bukavu wapate kuwa na vikartasi mhimu vya kuwaruhusu kwendesha kazi yao bila shaka.

Anena hayo katika mkutano aliyoendesha na viongozi wa watembeza pikipiki na wa madreva baada ya vurugu kujitokeza mjini Bukavu hii juma tano 19 mei . Watembeza pikipiki wakipinga msako barabarani.

Msako ili kulazimisha watumiaji wa barabara kuwa na vikartasi vya kuwaruhusu kufanya kazi yao tukitaja kikartasi cha orodha yaani plaque d’immatriculation kwa lugha la kimombo na kile cha kuruhusu kutembeza yaani permis de conduire kwa lugha la kimombo.

Ndani ya mkutano, wenyeji pikipiki na gari wameonyesha kupandishwa kwa beyi ya vikartasi hivyo. Wakionyesha kuwa kikartasi cha orodha yaani plaque d’immatriculation ni dola za marekani 25 mjini Goma ijapo mjini Bukavu ni dola 40 za marekani. Na kwamba kikartasi kinachoruhusu kutembeza mjini Goma ni dola 15 ijapo Bukavu ni dola 25 za marekani.

Kwa kutekeleza amani jimboni Kivu ya kusini , waziri wa uchukuzi ametoa muda wa mwezi moja kwa watu hawa ili kuwa na vifaa hivyo vya kazi.

Ameongeza kuwa ataendelea na utetezi ili kutafuta namna ya kupunguza bei ila siyo vyepesi kwa bajeti ya mwaka 2021 kwani pesa hizo zahesabiwa ndani.

Akisema kwamba hayo yatatekelezwa kwa bajeti ya mwaka wa 2022.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire