Goma : Bi Olive Lembe KABILA ajitowa kwa kuwapa misaada wahanga wa mripuko wa volkeno Nyiragongo kama desturi

Bi Olive Lembe KABILA mama wa roho

Bi Olive Lembe KABILA ambaye mumewe alikuwa raisi wa DRC miaka iliopita ametowa hii juma mosi tarehe 10 julai misaada kwa ma mia ya jamaa zinazokaa ndani ya kempi ipatikanayo kunako shule Kahembe wilayani Nyiragongo. Hawa wakiwa wahanga wa mripuko wa volkeno Nyiragongo wa tarehe 22 mei iliyopita.

Zaidi ya jamaa elfu mbili ziishimo ndani ya kempi zimetolewa vitu mkono mkononi naye mke wa Raisi wa zamani Bi Olive Lembe KABILA, namna ya kuwapanguza macozi. Kitendo ambacho ni lengo pia la serkali ya DRC.

Wahanga wapewa uji nzito, vikwembe n’a kiwango cha pesa ili kuendelesha maisha ambayo yalizorota zaidi tangu mripuko huo.

Baada ya mcana kati Bi Olive Lembe KABILA alitowa hekta mia moja kwa wahanga wa mripuko huo wa tarehe 22 mei 2021. Kila aliepoteza nyumba alipewa mita 20 dhidi ya 15 hata kumjengea makao.

Kazi zitasapotiwa na shirika Initiative Plus Olive Lembe KABILA. Kutokana na shirika lenyewe kazi zitaanza hapa karibuni kwani mama huyu akiitwa mama wa roho anaendelea kukerwa na maisha ya wahanga hawa ambayo pia ni hitaji ya viongozi wa DRC.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire