Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Promesse Matofali anena kuwa kazi za kikao zaendeshwa hadi hatua itakapochukuliwa na kutangazwa naye Prezidenti wa chama chao.
« Siwezi kutamka jambo lolote mbele ya Prezidenti wa chama kwa kuwa mazungumzo yanaendelea mjini Lubumbashi. Tunarudi hapa Goma ili kuendelesha kazi hiyo hadi hatua itakapochukuliwa. Najua Prezidenti atafwata maoni ya walio wengi ndani ya chama » anena Mubunge jimboni Promesse Matofali.
Mwanabunge huyu anena kuwa alifasiria ndani ya kikao jisi hali yazorota jimboni Kivu ya kaskazini kijamii , uongozi wa kijeshi bado kufaulu. Akigusia mauaji kila leo Béni na Ituri.
« Tuliambia Prezidenti kwamba wafanya siasa wa Muungano Union sacrée hawajihusishi na hayo yote. Hakuna majengo bora na hii itapelekea tuondoke ndani ya Muungano Union sacrée. Hatuwezi endelea na watu wasio kubali shauri » anena Mwanabunge huyu.
Promesse Matofali asisitiza kwamba chama chake kina lenga matakwa ya raia na ndio maana kiliondoka mbeleni ndani ya utawala wake Raisi wa zamani Joseph Kabila kwa kuwa utawala huo ulifanya masikio kuwa magumu.
Mwishowe anena kufurahishwa na hatua ya wanabunge wa taifa ambao wameamuwa kuondoka bungeni wakionyesha kuwa hadi sasa uongozi wa kijeshi haujafaulu.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.