Goma: Mathieu Batumike Mpinike anena kuunga mkono Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI kwa kazi za maendeleo nchini DRC na serkali kwa jumla

Mwakilishi wa chama cha kisiasa Les républicains Kivu ya kaskazini na kusini

Mwakilishi wa chama cha kisiasa Les républicains Kivu ya kaskazini na kusini Mathieu Batumike anena kuuunga mkono kazi za maendeleo zake Raisi wa DRC pamoja na serkali ya nchi hiyo.

Alinena hayo wakati wa sherehe za kuzinduwa jengo kubwa la shirika lihusikalo na mafunzo ya kiufundi nchini INPP maarufu juma tatu tarehe 29 novemba 2021 mjini Goma.

Jumba lilijengwa kwa msaada wa nchi ya Ufransa ambayo inasema kuhusika na maendeleo ya DRC , kupitia mtamshi yake balozi wa Ufransa nchini DRC.

Wakishiriki kwenyi sherehe liwali mwana jeshi wa jimbo la kivu ya kaskazini Constant NDIMA na wasaidizi wake, mawaziri kadhaa toka Kinshasa wakisindikiza waziri ahusikae na kazi, kijamii Bi Claudine Ndusi.

Kwake Mathieu Batumike, Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo imeanza moja kwa moja kubadili picha yake ya hapo awali kimaendeleo.

 » Tulikuwa tukitoa machozi ili serkali ya jimbo ipate jengo nzuri na sasa tumelipata .Hii ni furaha kwetu.anena mwana siasa wa chama Les républicains chake Léon Kengo wa dondo.

Mwishowe aomba raia jimboni Kivu ya kaskazini kulinda vema jengo hilo kwa manufaa ya wote.

Juvénal Murhula

K

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire