Jenerali wa brigedi Ilunga Mpeko kamanda makamu huyo apatikana mjini Beni jimboni Kivu ya kaskazini tangu juma pili baada ya mcana kati.
Habari kutoka jeshi, sekta ya operesheni Sokola1 eneo hilo zaangazia kwamba Jenerali huyo apatikana pa Béni ili kuchunguza na kuandaa vikosi vyenyi kuhusika na kuwagonga wanamugambo ADF.
Kwa mhusika na operesheni kwenyi vikosi vya ardhini akizungumza na kamanda wa operesheni Sokola1 pamoja na afisa wengine wa kijeshi ili kufahamu gisi operesheni zaendeshwa na shida zinazokumba askari jeshi kwa kutotekeleza amani kaskazini mwa Kivu ya kaskazini, ambako usalama mdogo unasababisha vifo.
Katika majadiliano , Jenerali wa brigedi Ilunga Mpeko aliwapa moyo vikosi vilivyo tumwa huko kwa juhudi na hatua ya kuwasaka maadui ili kutekeleza amani eneo hilo la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.