Bukavu : Shirika za raia jimboni Kivu ya kusini hazina kauli moja kuhusu maandalizi ya mji bila kazi tarehe mosi machi 2022

Ville de Bukavu

Wakati shirika la raia mjini Bukavu lilikuwa lilikuwa likichukua hatua ya mji bila kazi kwa kuomba raia wabaki makwao tarehe mosi machi hapa karibuni, upande wake shirika nyipya la raia NDSCI jambo hilo haliwa husu kwa raia waishi wakitafuta siku kwa siku kutokana na hali ya maisha ambayo ni ngumu.

Bwana Jackson Kalimba wa shirika la raia mjini Bukavu aliyesahini ujumbe anena kuwa hali ya uongozi wa jimbo inayumbayumba kiasi . Huyu agusia malipo kiasi ya shule za sekondari, barabara mbovu mjini na jimboni kote, usalama mdogo kila leo na kadhalika. Akiongeza kwamba uongozi wa mahali hauambatane na ukabila, huenda wamoja huzani ni jambo la ukabila.

Upande wa Shirika Nyipya la raia, watu waishi hali ya shida, na ndio maana hakuna umuhimu wa kujiunga kwa hatua hiyo. Kwani kuna aina nyingi ya mtu kudai haki. NDSCI CUMVI ya CONGO yaomba raia kutoanguka ndani ya mtego ya wafanya siasa ambao wapigania faida zao wenyewe. Shirika Nyipya la raia laomba wafanya siasa kuwa na zamiri safi, wakae pamoja na kuzungumza kuhusu ujenzi wa jimbo la Kivu ya kusini kwani yawezekana.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire