
Tunafanya utetezi siku kwa siku kuhusu usalama mdogo jimboni Kivu ya kaskazini. Napatikana ndani ya kamisheni husika na ulinzi pia usalama bungeni.
Hii ni matamshi yake Mwanabunge wa taifa Magy Rwakabuba akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma. Huyu akitokea mjini Kinshasa hii juma pili tarehe 6 machi 2022.
Mchaguliwa wa Rutshuru aongeza kuwa kuna matumaini kwa uongozi wa kijeshi, kwa kutafuta suluhu kuhusu usalama mdogo unaokumba Kivu ya kaskazini na Ituri.
Alipokelewa kwa shamra shamra na wanamemba wa chama chake , mwanabunge huyu wa taifa anena pia kwamba akuja kufanya kazi za kisiasa na kuhuzuria kwenyi sherehe za wanawake tarehe 8 machi.
« Inabidi kujuwa kwamba tarehe 8 machi kila mwaka akina mama washerekea siku kuu yao ulimwenguni. Nakuja pia kushiriki kwenyi sherehe za akina mama jimboni Kivu ya kaskazini », asisitiza mwanabunge wa taifa Maguy Rwakabuba.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.