Nyiragongo : Mwili usio na uhai wa mtu wa miaka takriban kati ya ishirini na tisa na thelasini waogotwa

Shirika la raia la Nyiragongo

Mwili usio na uhai wakutwa asubui ya juma nne tarehe 8 machi kwenyi kijiji Ngangi ya kwanza eneo la Munigi wilayani Nyiragongo Kivu ya kaskazini.

Duru toka shirika la raia la mahali ni kwamba mhanga aliyezaniwa kuwa na umri wa miaka kati ya 29 na 30 alikutwa na alama ya vidonda mwilini bila kujuwa chanzo cha mauaji.

 » Tunalaumu mara tena mauaji kwetu na kuomba viongozi kujihusisha ili kukomesha tabia hiyo anena Adolphe Shukuru kiongozi wa shirika la raia pa Munigi kwenyi wandishi habari.

Kumbukeni kwamba visa vya mauaji na miili zisizo na uhai kuogotwa ni kila leo wilayani Nyiragongo jimboni Kivu ya kaskazini.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire