Nyiragongo : Raia wa vijiji Kiziba 1 na Bugamba1 waporwa pesa na vitu vyenyi samani kubwa

Dola mia tatu za marekani, televisheni, simu za mkononi na vifaa vingine vya nyumbani viliporwa na kundi ya wevi arubaini eneo la Munanira Kijiji Kiziba 1 na Kanzana Kijiji Bugamba1 wilayani Nyiragongo.

Duru zetu zanena kwamba ni kundi la wevi ndilo liingia ndani ya nyumba tatu eneo hizo na kupora dola mia 5 za marekani na vitu vyenyi samani kubwa.

Tulikuwa tukijiswali nini chanzo cha usalama mdogo pa Nyiragongo hatupate jibu. Tunaomba viongozi kutulindia usalama laeleza shirika la raia la mahali.

Tukumbushe kwamba ni siku nyingi tangu kuripotiwa kwa visa vya wizi wilayani Nyiragongo na hata mjini Goma.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire