Kivu ya kusini/ Kabare : Mwanasheria Daniel Lwaboshi aona umuhimu wa maendeleo ya kudumu wilayani mwake

Shule kadhaa eneo la Luhihi wilayani Kabare zimepokea mabati kumi kila moja pamoja na saruji ajili ya ujenzi.

Mwakilishi wa chama UNC Kivu ya kusini mwanasheria Daniel Lwaboshi achukuwa hatua ya kuboresha maendeleo huko Luhihi wilayani Kabare eneo lake la kuzaliwa.

Shule za msinji ambazo zilizopokea vifaa hivyo ni Lomera, Murhobo na Mugererebo shule ambako kiongozi huyo alianza kuelimika. Kila shule lilipokea mabati kumi ili ya kujenga darasa nyipya.

Kiongozi wa shule la msinji Lomera Jackson Bavurhe moja wa waliopokea msaada ashukuru kwa niaba ya wote kitendo hicho kizuri cha Mwanasheria Daniel Lwaboshi

Tukumbushe kwamba kanisa pamoja na vituo vya afya havikusahaulika naye mtu huyo wa moyo mwema.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire