Goma: Francine Cizungu yupo ziarani Kivu ya kaskazini na kusini ili ya kuchochea kazi

Mratibu wa shirika lisilo la kiserkali husika na huduma kwa vijana wasio na kazi na hata wajane Francine Cizungu apatikana jimboni Kivu ya kaskazini na kusini tangu ijumaa tarehe 1 aprili 2022 toka mji mkuu Kinshasa. Mbele ya wandishi habari mjini Goma, alifahamisha kwamba ni katika lengo la kuchochea kazi za chama chake UNC na hata zile za AJMAC shirika ambalo yeye ni mratibu.

Francine Cizungu alipata fursa ya kusalimu Prezidenti wa chama UNC Vital Kamerhe. Akinena kwamba atajielekeza pa Nyangezi, Walungu ajili ya kazi na baadae kurudi mjini Goma.

Kiongozi wa kamati ya wazee wenyi busara Casinga Ntumulo Zachée wa shirika AJMAC aliyempokea anena kwamba wataweza kutapanya popote kazi za chama UNC zenyi kuzaa maendeleo.

« Nampokea msichana wangu Francine Cizungu ambaye tutafanya safari pamoja Nyangezi, Walungu, Izege na hata Uvira. Tuko na kazi kubwa ya kufanya kupitia shirika AJMAC, » afasiria kiongozi huyu wa kamati ya wazee wenyi busara.

Casinga Ntumulo aangazia kwamba shirika AJMAC ni moja wapo miongoni mwa mashirika za chama UNC, na kupitia chama hicho watatumikia nchi.

 » Sisi ni vijana shujaa, tunaamini kufikia lengo. Prezidenti wa chama UNC Vital Kamerhe ameachiliwa huru, kwanza hayuko tena jelani. Sisi hatuzembeye, tunatowa shauri na hata busara kwa vijana, alikomesha mtamshi yake Casinga Ntumulo Zachée mwenye kiti wa kamati ya wazee wenyi busara ya shirika AJMAC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire