Goma: Akijielekeza ziarani mjini Bukavu ajili ya afya mwanabunge wa taifa Didier Okito Lutundula ajibu kwa maswala za wandishi habari

Akihojiwa na wandishi habari hii ijumaa tarehe 22 aprili 2022 kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, mchaguliwa wa mji wa Bukavu, Didier Okito anena kuja mjini Bukavu ajili ya hali ya afya yake.

Kwa nini hakuna jibu kuhusu kibarua alicho kituma kwake waziri wa mambo ya ndani Daniel Aselo, huyu ahakikisha kwamba jibu litapatikana, na kwamba bunge la taifa linakuwa na kazi chungu tele, mfano wa sheria kuhusu uchaguzi ambayo haijatekelezwa vilivyo na mengineo.

Kuhusu uongozi wa kijeshi ambao matokeo yanaonekana kuwa mbovu Didier Okito anena kwamba ingawa Raisi wa DRC hajanena lolote lile inamaanisha kwamba shida yaendelea kuonekana maeneo ya uongozi wa kijeshi.

Tufahamishe kwamba mwanabunge wa taifa Didier Okito mchaguliwa wa mji wa Bukavu aliweza andika kibarua dhidi ya waziri wa kwanza makamu na wa mambo ya ndani Daniel Aselo, akimshutumu uongozi mubaya ya majimbo na sekta zingine chini ya uongozi wake.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire