Kivu ya kaskazini: Wahanga wa vita wilayani Rutshuru watapokea msaada toka serkali

Msaada wa chakula na vifaa vingine utapelekwa kwa wahanga wa vita pa Rutshuru, namna ya serkali ya DRC kuwapa pole wakaaji wa eneo hilo lenyi kukumbwa na vita.

Matamshi ni yake mwanabunge wa taifa Jean Luc Mutokambali mbele ya wandishi habari mjini Goma juma pili tarehe 24 aprili akitokea mji mkuu Kinshasa.

« Ni kawaida kuja na msaada ya wandugu ambao wamekumbwa na vita wilayani Rutshuru. Nakuja na ujumbe wa hongera na kuomba wakaazi waungane bega kwa bega ili kupiganisha adui, wakiwa na matumaini kwa serkali », anena mwanabunge Jean Luc Mutokambali.

Kuhusu kuongezewa mhula kwa uongozi wa kijeshi, huyu anena kwamba angojea matokeo ya ucunguzi kuhusu uongozi huo wa zarura. Akisisitiza kwamba ziara yao ni kuwapongeza raia ya Rutshuru.

Akihojiwa kama wanabunge waendesha kazi yao vizuri ama la.

« Kila mwanabunge anayefahamu kazi yake kisheria afanye awezayo. Ila kazi ya mwanabunge siyo kufanya vita, vita ni ya jeshi la taifa », asisitiza mwanabunge Jean Luc Mutokambali.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire