DRC/ CENI: Denis KADIMA Prezidenti wa tume huru ya uchaguzi ameanzisha kazi kuhusu kanuni zitakazo sindikiza sheria ya uchaguzi

Prezidenti wa tume huru ya uchaguzi CENI Denis KADIMA.

Prezidenti wa tume huru ya uchaguzi nchini DRC Denis KADIMA alianzisha hii juma tano tarehe 20 julai 2022 mjini Kinshasa, semina ya kutengeneza upya sheria kuhusu uchaguzi nchini DRC.

Alisindikizwa na makamu wake Bienvenu Ilunga, Denis KADIMA afahamisha kwamba muda wa siku sita, watalaam wa sheria, watatengeneza upya sheria ya uchaguzi kupitia kanuni zitazotekelezwa.

 » Nashukuru timu letu la wana sheria kuhusu ripoti yao, wakati ilikuwa ikicunguzwa na kamisheni husika na siasa, uongozi na sheria bungeni. Nataka kwenyi kikao bungeni, na nafasi zingine, sheria izungumziwe ili kutekeleza kazi, » aeleza mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi CENI.

« Kazi kuhusu sheria hiyo, ziliweza kufanyika kwa uhakika, na ndivyo itaendelea ili kutowa mwanga kuhusu kanuni, itakayopelekea wachunguzi wa sheria kuwa na kauli moja, » anena Denis KADIMA.

Prezidenti makamu Bienvenu Ilunga aliomba washiriki kikao kutowa kwenyi tume huru ya uchaguzi, buku la kanuni ambayo inafasiria wazi sheria hiyo ili raia waelewe sheria kuhusu uchaguzi. Akiomba buku hilo la kanuni litumwe kwenyi kikao ya tume huru ya uchaguzi CENI, ili kuweka full stop na kuisambaza kama duru za CENI zaeleza.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire