Kivu ya kusini : watu hufariki dunia na wengine kujeruhiwa vikali wilayani Walungu

Ajali ya barabarani Bideka Mugogo

Habari toka wilayani Walungu jimboni Kivu ya kusini zaeleza kwamba ajali ya barabarani imejitokeza hii juma mosi tarehe 30 julai 2022, kwenyi barabara nambari 2.

Duru zetu zahakikisha kwamba ajali imejitokeza kwenyi barabara kati ya senta ya kazi za byashara ya Mugogo na Bideka. Na kwamba watu wengi wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa vikali.

Duru zingine zenyi kuaminika zanena kwamba na gari moja aina basi ambayo ilikuwa ikitokea mjini Bukavu na kujielekeza pa Kamituga, ndio iligonga pikipiki mbili na gari moja aina voiture kwa lugha la kimombo.

Waendesha pikipiki pamoja n’a wateja wao, na wengine wote waliojeruhiwa ndani ya basi, walipelekwa hima kwenyi hospitali pa Bideka, siyo mbali na nafasi ya ajali. Chanzo cha ajali bado kujulikana hadi sasa.

Media yako la ronde info yatowa pôle kwa jamaa zote zilizo kumbwa na msiba kutokana na ajali yenyewe.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire