Kivu ya kaskazini/ Masisi : Ajali ya barabarani ; watu wawili wafariki dunia na wawili kujeruhiwa vikali

Ajali ya barabarani Goma Sake.

Watu wawili wafariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vikali, kutokana na ajali iliyojitokeza karibu na Kijiji Nzulo, eneo la Kamuronza wilayani Masisi. Ni kwenyi barabara Goma Sake.

Duru zetu hueleza kwamba ni Lori moja aina Isuzu, ndio iligonga ingine aina Rv4. Watu wawili hupoteza maisha, na wengine wawili kujeruhiwa vikali.

Hayo yalifanyika juma tano kuamkia alhamisi tarehe 4 Agosti 2022 majira ya saa moja usiku. Miongoni mwa wahanga kiongozi wa shirika la kutoza ushuru DGI/ Masisi, na dreva wake aliyekuwa ndani ya Rv4 toka Sake.

Duru zaongeza kwamba watu wawili waliojeruhiwa wanapewa matibabu, kati yao muke wa prezidenti wa shirika ACCO wilayani Masisi.

Issa Libiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire