Alipowasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Christian Bahati Prezidenti wa shirika FOBAC alipokelewa kwa shamra shamra. Wanamemba wa shirika lake, viongozi kadhaa, akina mama mjini Goma, wasanii na vijana wengine wengi. Akinena kujihusisha na mambo ya kijamii.
Mwanzilishi wa shirika FOBAC Christian Bahati alishukuru wanamemba wake, kwa upendo na utashi wakiunga mkono maoni yake.
« Nafurahi kuhusu uhusiano wa leo. Ina maanisha kwamba tuna watu wenyi kustahili kwa ngazi za chini. Hii ni furahia kwangu. Nasema aksanti. Tuna maoni ambayo tutatekeleza. Tunajihusisha kila leo na maswala za kijamii, » aeleza Christian Bahati.
Akiongeza : » Niko mjini Goma ajili ya kazi za shirika. Kwa kweli, shirika FOBAC lapatikana mjini, Ila ni mara ya kwanza kwangu kufanya ziara. Nina mipango mikubwa kuhusu mji wa Goma na Bukavu. Tutahudumia watu wasiojiweza yaani wanyonge. Kuna kazi kubwa pia mjini Bukavu. Tutatumika kila leo ndani ya maswala za kijamii. Ni mhimu kuwahudumia wanao tupiliwa. Shirika Bahati Christian yaani FOBAC lapatikana ndani ya majimbo kadhaa nchini DRC. Kufika kwangu hapa ni kutowa msaada kwa watu hawa. Tutapata fursa ya kufasiria vijana, maana ya kuunda kazi, ukosefu wa kazi mashariki mwa DRC, inayotokana na kukosa uongozi. Sitafasiria yote hapa, shirika lina mengi ya kutekeleza, » aeleza Christian Bahati mbele ya wandishi habari.
Kiongozi huyu alijielekeza hima kwenyi jumba la wajane na yatima katani Majengo mjini Goma. Huku akitolewa malalamiko ya watu hawa.
Christian Bahati alitowa bahasha kwa wanyonge na yatima, namna ya kujibu kwa hitaji ndogo ndogo. Waliopokea msaada walinena kufurahi. Kiongozi husika na wajane na yatima alinena kwamba kitendo hicho kina maanisha upendo.
» Tunashukuru shirika FOBAC kuhusu mcango hii. Watu wengi wana mali ila hawana moyo ya kusaidia. Aksanti Christian Bahati. Hii ina maanisha upendo juu yetu. Tutaendelea na uhusiano. Naamini watoto hawa na hata wajane wana furaha kubwa, » atamka Sikuli Nyariba kiongozi wa senta hiyo.
Tufahamishe kwamba mbele ya kuondoka mjini Goma hadi Bukavu, Christian Bahati apanga kukutana na akina mama jimboni, vijana pamoja na makundi zingine za raia, ili kuelewa shida kijamii ambazo shirika FOBAC litajaribu kuleta suluhu.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.