Watu tano wakiwa wa jamaa moja wamepoteza maisha katika ajali ya moto kwenyi kata Kajangu, mtaani Kadutu mjini Bukavu jimboni Kivu ya kusini.
Duru zetu zaeleza kwamba ni wazazi na watoto watatu ndio wameunguwa ndani ya nyumba. Na kwamba moto ilijitokeza jamaa ikisinzia.
Duru hizo zaongeza kwamba chanzo cha ajali hakijajulikana bado.
Tufahamishe kwamba tangu mwezi juni nyumba mia moja tayari zimekwisha kuwaka moto ndani ya mitaa ya Kadutu na Ibanda, mjini Bukavu jimboni Kivu ya kusini.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.