Bukavu: Semina ya kubadili fikra kuhusu kuondoka kwa Monusco nchini DRC, bila kusukumwa likiwa jukumu lake

Imehitimishwa hii juma tano mjini Bukavu, semina ya kubadili fikra kati ya MONUSCO, viongozi wa serkali, miungano ya shirika la raia, wanaharakati, viongozi wa asili pamoja na raia wa mahali jimboni Kivu ya kusini.

Ndani ya mazungumzo hayo, Monusco pamoja na viongozi jimboni Kivu ya kusini, waliweza kubadili fikra kuhusu namna ya kuendelea na uhusiano bora, hadi kuondoka nchini DRC katika hali tulivu kwa Monusco, Huyu akiombwa kuchukua jukumu lake katika harakati hizo
.

Kazi ziliendeshwa muda wa siku mbili kunako hoteli Panorama, zikikusanywa katika mada tatu, zinazohusu; ukingo na usalama wa raia, mamlaka ya viongozi wa asili, utawala popote wa serkali, uongozi bora, kuchangia uchumi na kuboresha kazi za serkali.

Tukumbushe kwa jumla kwamba walioshiriki kwenyi kikao ni viongozi wa serkali, wabunge jimboni, mea wa mji, viongozi wa mita tatu ya mji wa Bukavu, viongozi wa asili, miungano ya shirika la raia, na wajumbe wengine toka shirika hilo, viongozi wa kidini na kadhalika.

Issa Libiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire