Rutshuru : Waasi wa M23 wavamia eneo nyingi wilayani humo siyo tu Bunagana( Aimé Mukanda)

Watu wengi huzani kwamba waasi wa M23 wavamia tu eneo la Bunagana wilayani Rutshuru ijapo wanazibiti pia eneo nyingi ndani ya vitongoji kadhaa.

Ndivyo amefahamisha Aimé Mukanda memba wa shirika la raia pia mtetezi wa haki ya binaadam pa Rutshuru. Huyu atowa mwanga kuhusu vijiji vyenyi kuvamiwa.

 » Eneo la Bweza ni Nyesisi, Nyekiliba, Binkenke, Ruvumu, Bukima, Shangi, Mutovu na Rutakara. Eneo la Jomba tunakuwa na Bunagana, Bigega, Ruginga, Mulongati, Gisiza, Nyambara, Kayenzi. Bugusa. Kinyamahura, Chengerero, Kabindi kwa Rushago na Ruvumba mpaka na Bweza na kijiji kimoja cha Busanza, » anena mtetezi huyo wa haki ya binaadam.

Tufahamishe kwamba vijiji hivyo vinavamiwa na waasi M23 tangu tarehe 13 juni 2022, ndani ya eneo tatu za wilaya ya Rutshuru jimboni Kivu ya kaskazini.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire