DRC : Tume huru ya uchaguzi CENI imefunguwa milango tarehe 16 na 17 januari ijapo ni siku kuu nchini

Tangazo toka Tume huru ya uchaguzi CENI limehakikisha kwamba milango ya shirika hilo ni wazi hata tarehe 16 na 17 januari, ambazo ni siku bila kazi, ili kukumbuka shujaa walio mwanga damu ajili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Jimbo kumi zilizo chaguliwa kuanzisha kazi hizo ziliendelea kufungua milango hii tarehe 16 na 17 januari ambazo hakuna kazi. Wakongomani wakikumbuka Mzee Laurent Désiré Kabila na Patrice Emery Lumumba.

Milango ilikuwa wazi tangu saa moja hadi saa kumi na moja jioni kwenyi majimbo kumi ambamo mwapatikana Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kwa hiyo, Tume huru ya uchaguzi CENI iliomba raia wanaoneza shurti, kwenda haraka na kujiorodhesha kwenyi senta za mahali.

Tukumbushe kwamba Tume huru ya uchaguzi CENI inaendelea na kazi za orodha ya wachaguzi, kwenyi eneo hilo tangu tarehe 24 disemba 2022.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire