Goma: Juliette Mughole Mbambu aomba akina mama wafanya biashara na hata wakulima kuepuka ukosefu wakiweka akiba

Akiwa ziarani mjini Goma, Prezidenti wa chama cha kisiasa ACLP Bi Juliette Mughole Mbambu alikutana na umati wa wanawake mjini humo, ambao walimlaki kwa shangwe na vigelegele.

Kwenyi jumba la mapokezi Bel air mjini Goma, Bi Juliette Mughole Mbambu alinena kuleta ujumbe wake Raisi Félix Antoine Tshilombo. Ambaye anataka kukomesha hali ya ukosefu ambayo inakumba akina mama walio wengi nchini DRC. Raisi akiweka mkazo kwa wanawake jimboni Kivu ya kaskazini wanao tatizwa kutokana na vita vya kila leo.

 » Inabidi akina mama yeyote yule awe na akiba kwenye benki la taifa CADECO, yaani mama mlimaji, mfanya biashara na kadhalika. Akina mama elfu moja wanahitajika kwa kipindi cha kwanza. Na baadae kuendelea. Mradi huu utafikishwa kote nchini DRC. Ila Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipendelea kwanza jimbo la Kivu ya kaskazini, lenyi matatizo chungu tele kutokana na hali ya vita vya kila leo. Ni majimbo Kivu ya kaskazini, Kivu ya kusini, Ituri na Tshopo ndizo zitahudumiwa mbele kulingana na shida zao, alieleza mfanya siasa huu Bi Juliette Mughole Mbambu Prezidenti wa chama cha kisiasa ACLP.

Juliette Mughole alifurahi kwa mapokezi ya akina mama jimboni Kivu ya kaskazini, akiwaomba kuzingatia tabia hiyo. Huyu akiomba akina mama hawa kwenda kujiorodhesha kwenye benki la taifa CADECO, mbele ya kutanana nawo kwa mazungumzo hii juma mosi tarehe 1 aprili mjini Goma.

Na katika mazungumzo hayo, akina mama wataelezwa kwa marefu, nawo watapewa fursa ya kujieleza kuhusu kazi wanazo zifanya.

Kulikuweko pia wafanya kazi kadhaa wa benki la taifa CADECO jimboni Kivu ya kaskazini, wakimsindikiza kiongozi wao.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire