Tangu zianzishwe operesheni za kuweka vikartasi kwenyi Tume huru ya uchaguzi, ili kugombea nafasi kunako bunge la taifa, wafanya siasa walimwangika kama mvua mbele ya raia. Wengi miongoni mwao wakitowa pesa, vyakula, vinywaji, mavazi na kadhalika kwa raia, wakisii waweze kuwachagua mara tena. Ijapo hawakufaulu vilivyo muda wowote waliopewa kwa kiboresha hali ya maisha ya raia, ambao wanakumbwa na shida chungu tele. Hali kiuchumi , kijamii na hata kiusalama huendelea kukwama. Mauaji ya kila aina, njaa na kadhalika.
Kuhusu hali hii, Profesa Daktari Dady Saleh pia mgombea kwenyi bunge la taifa, asii raia kuwa makini, kupokea kila watakacho kipewa na viongozi watesi, ila wasichaguwe. Wakikumbuka mateso waishimo ndani, inayosababishwa na wafanya siasa hawa.
Alinena hayo akizungumza na mwana ripota wa la ronde info hii juma nne tarehze 25 julai mjini Goma.
<<Nazani muda umetimu ili kuonyesha samani ya siasa inayohusu Kujitegemea, tumilukela, tusosange mosi. Inabidi raia kuchagua watu wanao stahili, Kulingana na sheria ya nchi, hakuna mtu anakataliwa iwe mwanabunge, ama mtu mwengine, hata kama ameiba kiasi kuja mbele raia, na kuomba achaguliwe mara tena. Pia hakuna kinacho mukataza kudanganya raia. Ingelikuwa kuna sheria inayohukumu wasema uongo, mtu kama huyu angetupwa jelani. Kwa sasa ni raia ndio waamuzi, wakijuwa akina nani wachaguwe, iwe mgombea wa uwingi wa uraisi, ama wa upinzani, ama wa shirika la raia, uamzi ni kwao. Mimi najisikia huru muda huu ninaji eleza kwa wakongomani. Wakongomani wenzangu; ni muda sasa wa kujuwa ni nani aliye chanzo cha mateso ambamo munaishi hadi leo. Ila nawaambieni kwamba miongoni mwa watesi wenu ni hawa viongozi almashauri wa vyama vya kisiasa. Zaidi ya asilimia themanini ya wakongomani 80% waishi katika hali ya umaskini , wakikosa chakula na hata malisho mabaya,>> anena Dady Saleh.
Akiongeza hali ya usalama mdogo. Zaidi ya kundi 150 zenyi kumiliki silaha, magaidi wa M23 pamoja na Rwanda, Uganda wakivamia kipande cha udongo wa nchi, kundi la wevi arubaini, utekaji nyara kila leo, usumbufu wa askari polisi na mengineo.
Kandideti kwenyi bunge la taifa Dady Saleh anena kwamba sisi sote tunayo jukumu ya kufanya maendeleo, ila ni kwa ngazi mbali mbali. Na kwamba walio ongoza nchi vibaya hawana nafasi yoyote mbele ya raia. Na kwamba hakuna mtu atakaye towa ushuhuda kuhusu uongozi bora wa DRC.
<< Hata kama kuna kazi ndogo ndogo zimefanyika ambazo ni kati ya asilimia 10 na 20 yaani 10 à 20% katika lugha la kimombo. Na hii ni kushindwa kinaganaga>> Dady Saleh akiwa mwenyi sikitiko
Akiongeza kwamba wabunge wengi wa taifa na hata wa jimbo walikwenda bungeni, ili kula asali na maziwa bila kufanya kazi.
<<Wanabunge hawa hawakufaulu kutekeleza hata maoni moja kuhusu sheria muda wa mhula bungeni. Na wote waliojaribu kuleta maoni yao kwa kutekelez sheria. walikoma bila kufikia lengo. Wengine wengi walikumbwa na usingisi ndani ya vikao bungeni, wakisahau kazi iliyowa peleka huko. Kwa jumla, walikubali kula rushwa, yaani gari zenyi samani kubwa, milioni ya dola za marekani, wakifurahisha viongozi wao wa kisiasa, na kufurahishwa na mateso ya raia, waliowatuma bungeni. Bila kusahau mishahara mikubwa ; mwanabunge akipokea dola za marekani elfu 21. Na kwa viongozi kadhaa wa serkali ni dola za marekani elfu 100, wengine elfu 200 na hata elfu 600 dola za marekani,>> aangazia mfanya siasa Dady Saleh.
Akisisitiza mishahara hiyo ipunguzwe kiasi, ijapo yeye ni mgombea kwenyi uchaguzi bungeni mwaka huu: Mwanabunge wa jimbo apate kupokea dola 250 za marekani yaani 250$, na ule wa taifa aweze kupokea dola 500 za marekani yaani 500$. Hiyo itapeleka walio wengi kutofanya siasa, wakifanya kazi zingine zenyi faida.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.