Goma: Kwake Kanali Blaise Bukasa uhusiano barabarani mwishoni mwa mwaka ni tangu tarehe 25 disemba 2023 hadi tarehe 6 januari 2024

Akihojiwa na wandishi habari mjini Goma, Kiongozi husika usalama barabarani Kanali Blaise Bukasa anena kwamba uhusiano barabarani mwishoni mwa mwaka ni tangu tarehe 25 disemba 2023 hadi tarehe 6 januari 2024. Akijibu pia kuhusu misongamano hapa na pâle mjini Goma, pamoja na hali ilioonekana barabarani wakati hii ya uchaguzi.

<<Kila mwisho wa mwaka, askari polisi husika na usalama barabarani hujihusisha na uhusiano barabarani yaani courtoisie routière katika lugha la kimombo. Sisi askari polisi husika tumeanza harakati hizo. Tumeshurtishwa kufanya uhusiano barabarani toka kamisa mkuu wa polisi jimboni Kivu ya kaskazini. Muda huo, tunakuwa tukiomba watumiaji wa barabara, kuheshimu sheria barabarani. Wakiwa wahanga wa vitendo vya usumbufu toka askari polisi barabarani, kueleza mapema kwa nambari 09726111, >>anena Kanali Blaise Bukasa.

Akihojiwa pia kuhusu hali ya misongamano kwenyi nafasi zimoja barabarani mjini mfano kwenyi soko Alanine, hospitali kuu ya Goma na kwenyi mashanganjia INSTIGO, Kiongozi husika anena kwamba makosa zinapatikana pande zote, upande wa watumiaji wa barabara na hata askari polisi husika.

<<Tukianzia kwa wenyi kutumia barabara, wengi miongoni mwao hawana mafunzo kuhusu kanuni barabarani. Vikartasi vinavyo ruhusu mtu kutembeza barabarani vinatolewa kinyume na sheria. Mtu anatolewa kikartasi pasipo uchunguzi ama mtihani. Baadae huonyesha kikartasi hicho pasipo mafunzo. Ndio maana watu wengi watembeza wakiwa walevi na kadhalika. Na hiyo yasababisha ajali nyingi na misongamano kila leo>>, aeleza Kiongozi husika usalama barabarani Kanali Blaise Bukasa.

Upande wa askari polisi, Kiongozi huyo anena kwamba kuna wale ambao ni wana wapotevu ndani ya polisi. Wakifanya kazi pasipo kushikilia sheria. Na kwa hiyo, askari polisi hawo wanafunzwa usiku kama mchana ili waweze kuendesha kazi zao wakiheshimu sheria.

Kutokana na wadadisi wa mambo, ilionekana upungufu wa visa vya ajali za barabarani tangu mwanzo wa kampeni hadi wakati wa kupiga kura, Kiongozi husika na usalama barabarani alijibu kwamba hiyo ilitokana na tartibu za mafunzo aliopewa katika kazi ya ulinzi ya usalama barabarani. Akiheshimisha sheria iliyopangwa. Na ndio maana visa vya ajali havikuonekana vingi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire