Goma : Hali ni shwari katani Kahembe ijapo idadi ndogo ya askari polisi eneo hilo (Célestin Tulinabo)

Exif_JPEG_420

Kiongozi wa kata Kahembe mtaani Goma Célestin Tulinabo aomba kuongeza idadi ya askari polisi ili kuchunga ofisi yake. Pamoja na hayo kuomba idara jimboni husika na mkaaji , kufanya yote ili kugawa njia ndani ya eneo kadhaa za kata hiyo ya mtaa wa Goma.

Alinena hayo hîi juma nne tarehe 27 februari 2024 mjini Goma mbele ya wandishi habari wa mahali.

Akijibu pia kuhusu hali ya usalama, huyu alinena kwamba hali ni shwari katani mwake. Na kwamba ni moja ya kata mjini Goma ambamo hamupatikane kundi la wevi arubaini yaani 40 voleurs. Ijapo kundi hilo linaripotiwa karibu kunako kata nyingi mjini Goma.

Kuhusu mbinu anazozitumia ili ya kutekeleza usalama eneo lake, huyu anena kwamba aliweza kugawa vyombo vya mawasiliano kwa viongozi wake akianzia kwa ule wa chini na kupanda. Viongozi hawo wana pia uhusiano bora. Kila saa za jioni wajitembeza ndani ya kata nzima ili kuchunguza hali ilioko. Na hiyo imepelekea kimya ndani ya kata.

Kuhusu kukarabati kata, kiongozi wa kata Célestin Tulinabo aomba idara husika n’a mkaaji kufanya yote iwezekanayo ili kufugua njia ndani ya eneo lake, kama ilivyo ahadi. Kwa kuwa nafasi nyingi zaonekana kuzibwa. Inabidi zifunguliwe ili kuwe na hewa nzuri katani.

Kuhusu kuonekana kwa jambazi wamoja ndani kata hiyo, bwana Célestin Tulinabo anena kwamba kila mara washika watenda maovu hawo. Ila wanapo wapeleka kwenyi askari polisi, wakati mwengine waachiliwa, wakiendelea kuzurura katani.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire