DRC: Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO amekubali mara tena mazungumzo na Paul KAGAME

Raisi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO amekubali mara tena kukutana naye mwenziwe wa Rwanda  Paul KAGAME, ili ya kutafuta suluhu kwa ujeuri mashariki mwa DRC.

Kutokana na waziri husika n’a mambo ya nje wa Angola  Tete Antoinio, Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO amekubali hayo hîi juma nne tarehe 27 februari 2024, mbele ya mpatanishi wao  Raisi wa Angola Joaô Laurençon, nchini Angola.

Wakati huo, Félix Antoine TSHISEKEDI ametowa shurti zake ili kukutana mara tena na Paul KAGAME. Akiomba Raisi wa Angola kutumika kuhusu shurti zingine ili kufikia mazungumzo hayo.

Tukumbuke kwamba wakati wa kàmpeni ya uchaguzi, Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO alikataa kinaganaga kwamba hatakutana mara tena naye  Paul KAGAME wa Rwanda, hadi itakapo fika uamzi wa mwisho mbele ya Mwenyezi Mungu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire